1. K: Pote atawala nani? W: Pote atawala nani? K: Ni nani? W: Ndiye Mungu Mwenyezi. 2. K: Msifuni Mungu wetu, W: Msifuni Mungu wetu K: Yu Bwana, W: Vyote ni mali yake. 3. K: Mwumba jua nao mwezi, W: Mwumba jua nao mwezi? K: Na nyota W: Kwani anayo enzi. 4. K: Sasa wewe roho yangu, W: Sasa wewe roho yangu K: Kubali, W: Nyenyekea kwa Mungu. 5. K: Roho isiyotulia, W: Roho isiyotulia, K: Na Bwana, W: Haitapata raha. 6. K: Amemtuma Mwana wake, W: Amemtuma Mwana wake, K: Yesu Kristo, W: Ili atuokoe. 7. K: Amemshinda shetani, W: Amemshinda Shetani, K: Na dhambi, W: Na kutupa uzima. 8. K: Asimamisha agano W: Asimamisha agano, K: La Bwana, W: Haleluya, ee Yesu. 9. K: Dunia wamsifu, W: Dunia wamsifu K: Kwa shangwe, W: Kwa kuwa hututunza. 10. K: Watawala na raia, W: Watawala na raia, K: Na waje, W: W...