252. Mungu Twakuimbia
1. Mungu twakuimbia,
tunasifu nguvu zako.
Tunakuangukia
kwa kuona mambo yako.
Ulivyokuwa kale
utakuwa milele.
2. Nchi zote na mbingu,
na majeshi yao yote,
wote wakuimbia.
Hata wingi wa malaika
wakusifu mbinguni
Ee Mungu mtakatifu.
3. Bwana wetu Mungu mkuu
Mtakatifu mwenye enzi,
u shujaa na Mwokozi,
Mbingu, viumbe, bahari
zimeumbwa na wewe,
zote zinakusifu.
4. Duniani popote
watu wako wakusifu,
ni wazee na watoto
wakuimbiao Baba,
wamsifuo Mwanao
na Roho Mtakatifu.
5. Bwana uturehemu,
utupe baraka yako.
Neema yako iwe kuu,
kwao wakuogopao.
Tunakutumaini,
hivi hatupotei!
Comments
Post a Comment