276. Nina Haja Nawe
1. Nina haja nawe kila saa;
Hawezi mwingine kunifaa.
Yesu nakuhitaji
vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi
nakujia.
2. Nina haja nawe; kaa nami,
na maonjo haya, hayaumi.
Yesu nakuhitaji …
3. Nina haja nawe, kila hali,
maisha ni bure, ukiwa mbali,
Yesu nakuhitaji …
4. Nina haja nawe, nifundishe
na ahadi zako zitimize.
Yesu nakuhitaji …
5. Nina haja nawe, mweza yote,
ni wako kabisa siku zote.
Yesu nakuhitaji …
Comments
Post a Comment