265. Mganga Wetu ni Karibu
1. Mganga wetu ni karibu,
hashindwi na uchawi,
upendo wa kutufia
ni dawa yake njema:
Imbeni na malaika,
Jina lenye furaha,
ndilo la kutukuka,
Jina lake Yesu.
2. Hatuna utengamano
wala uzima hata,
ila Yeye kweli ndiye
aliyetupumzisha:
Imbeni …
3. Machukio na ugomvi
ametuondolea,
twende na kumtegemea
hata kwake mbinguni:
Imbeni …
4. Hulioni Jina tamu
lake Mwokozi Bwana?
Atuletea wokovu,
hatashindwa na kufa:
Imbeni …
5. Hilo ndilo nipendalo,
linipalo uzima,
linanipasa kwa kweli,
liheshimiwe nami:
Imbeni …
6. Kila mume asimame,
sifa zake zivume,
wanawake na washike
kusifu Jina lake:
Imbeni …
7. Na vijana wote pia,
awapendao sana,
waje kwake, wawe wake,
wamtumikie yeye!
Imbeni …
8. Nasi tutakapofika
mjini kwake mbinguni,
tutaimba kwa furaha
sifa zake milele!
Imbeni …
Comments
Post a Comment