Posts

242. Tumsifu Mungu Bwana

1. Tumsifuni Mungu     Bwana Mtakatifu     anatawala vizuri popote,     asiyekubali wabaya watutese,    tumsifu Mungu wetu,     hakutusahau. 2. Tulipoumia alituokoa,     atusaidia tulio wake.    Nasi twawashinda     maadui popote,    sababu Bwana wetu     anatuongoza. 3. Twamsifu Mwenyezi     aliye mbinguni.     Twamwomba:    “Uzidi kutubariki,     mwovu asipate      kutudhuru kwa hila,”     twasifu Jina lako,      Mwokozi wetu mkuu.

243. Wazima Wote Wamsifu

Wazima wote wamsifu Bwana,  Wazima wote wamsifu Bwana!  Msifu Bwana, Msifu Bwana.  Nyumbani mwake tumshangilie  nguvu zake za juu tuzisifu!  Wazima wote, msifu Bwana,  wazima wote, wazima wote,  Wamsifu Bwana! Wamsifu Bwana! Kwa filimbi na baragumu  na vinubi hata zeze na ngoma  wamsifu Bwana, wamsifu Bwana.  Wazima wote, wamsifu Bwana  baragumu na filimbi   wamsifu Bwana,  Ee, Bwana wa Majeshi. Haleluya. 

244. Kristo Usituondoke

1.  Kristo usituondoke      sababu mchana waisha,     mwanga wa Neno la Mungu     usiuzimishe kwetu! 2.  Nyakati hizi za mwisho      tusaidie kushika      Neno la huruma yako      nalo fumbo takatifu.  3.  Kundi lako ulilinde      ulikusanye mwenyewe,      libariki Neno lako,       litangaziwe popote! 4.  Mambo na mashauri yote      si yetu ila ni yako,     kwa hiyo wasimamishe      wanaokutegemea. 5.  Neno lako ngome kubwa,     hata boma la makundi;      kwa Neno lako tulishe      tusitafute mengine!

245. Huruma Zako Ni Nyingi

1. Huruma zako ni nyingi     Yesu siku kwa siku,     mapenzi yako yapita     kiasi cha maneno! 2. Watupenda na kutoa     damuyo msalabani,    watakatifu wapenda     kumwona Mungu wao. 3. Watupenda tangu mwanzo,     ni mwanzo wa furaha.     Mwisho wa kutegemea    ni kukuona wewe. 4. Tujue, Bwana, Mkombozi,    utupendavyo sasa     mpaka tutakapokufa,     tutakuona wewe.

246. Wenzetu Leo Hii Twawaaga

1. K:  Wenzetu leo hii         twawaaga kweli    W:  Muende salama.     K:  Njiani muwe na         safari ya heri;    W:  Mlindwe na Bwana.      K:  Kweli     W:  Mfike salama.      K:  Nyumbani     W:  Muone jamaa. 2. K:  Tunayo huzuni,         furaha, sababu     W:  Ninyi mwatutoka.      K:  Lakini tunayo         imani kwa Mungu     W:  Kwamba tu pamoja,     K:  Katika    W:  Sala za imani.     K:  Twaona    W:  Umoja wa kweli. 3. K:  Twamsifu Bwana         kwa kazi yenu njema    W:  Mliyoifanya.     K:  Twamwomba na huko      ...

247. Namwandama Bwana

1. Namwandama Bwana    kwa alilonena,    njia yangu huning’azia;     nikimridhisha     atanidumisha     taamini nitii pia.           Amini utii njia           pekee ni hii           ya furaha kwa Yesu:           amini ukatii. 2. Giza sina kwangu     wala hata wingu.    Yeye mara huviondoa     woga, wasiwasi,    sononeko, basi;     Huamini natii pia.           Amini utii … 3. Masumbuko yote,     sikitiko lote;    kwa mapenzi hunilipia;    Baa, dhara, dhiki,    vivyo hubariki.     Niamini nitii pia.           Amini utii … 4. Mimi sitajua     raha sawasawa     ila yote Yesu kumpa;    napata f...