246. Wenzetu Leo Hii Twawaaga
1. K: Wenzetu leo hii
twawaaga kweli
W: Muende salama.
K: Njiani muwe na
safari ya heri;
W: Mlindwe na Bwana.
K: Kweli
W: Mfike salama.
K: Nyumbani
W: Muone jamaa.
2. K: Tunayo huzuni,
furaha, sababu
W: Ninyi mwatutoka.
K: Lakini tunayo
imani kwa Mungu
W: Kwamba tu pamoja,
K: Katika
W: Sala za imani.
K: Twaona
W: Umoja wa kweli.
3. K: Twamsifu Bwana
kwa kazi yenu njema
W: Mliyoifanya.
K: Twamwomba na huko
muendako kwenu
W: Muwe waaminifu
K: Kazini
W: Muwe mashahidi.
K: Daima
W: Muwe na ushindi
4. K: Kwaheri ya heri,
wapendwa, twaomba
W: Tuonane tena
K: Na Mungu Baba
atulinde sote
W: Tuwapo popote
K: Pengine
W: Tusipoonana,
K: Tuonane
W: Kwake kwa milele.
Comments
Post a Comment