244. Kristo Usituondoke

1.  Kristo usituondoke 

    sababu mchana waisha,

    mwanga wa Neno la Mungu

    usiuzimishe kwetu!


2.  Nyakati hizi za mwisho 

    tusaidie kushika 

    Neno la huruma yako 

    nalo fumbo takatifu. 


3.  Kundi lako ulilinde 

    ulikusanye mwenyewe, 

    libariki Neno lako,  

    litangaziwe popote!


4.  Mambo na mashauri yote 

    si yetu ila ni yako,

    kwa hiyo wasimamishe 

    wanaokutegemea.


5.  Neno lako ngome kubwa,

    hata boma la makundi; 

    kwa Neno lako tulishe 

    tusitafute mengine!

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu