245. Huruma Zako Ni Nyingi

1. Huruma zako ni nyingi 

   Yesu siku kwa siku, 

   mapenzi yako yapita 

   kiasi cha maneno!


2. Watupenda na kutoa 

   damuyo msalabani,

   watakatifu wapenda 

   kumwona Mungu wao.


3. Watupenda tangu mwanzo, 

   ni mwanzo wa furaha. 

   Mwisho wa kutegemea

   ni kukuona wewe.


4. Tujue, Bwana, Mkombozi,

   utupendavyo sasa 

   mpaka tutakapokufa, 

   tutakuona wewe.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu