247. Namwandama Bwana
1. Namwandama Bwana
kwa alilonena,
njia yangu huning’azia;
nikimridhisha
atanidumisha
taamini nitii pia.
Amini utii njia
pekee ni hii
ya furaha kwa Yesu:
amini ukatii.
2. Giza sina kwangu
wala hata wingu.
Yeye mara huviondoa
woga, wasiwasi,
sononeko, basi;
Huamini natii pia.
Amini utii …
3. Masumbuko yote,
sikitiko lote;
kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki,
vivyo hubariki.
Niamini nitii pia.
Amini utii …
4. Mimi sitajua
raha sawasawa
ila yote Yesu kumpa;
napata fadhili
na radhi kamili,
niamini nitii pia.
Amini utii …
5. Nitamfurahia
na kumtumaini,
safarini hata nyumbani;
agizo natenda;
nikitumwa huenda,
huamini natii pia.
Amini utii …
Comments
Post a Comment