1. Nina haja nawe kila saa; Hawezi mwingine kunifaa. Yesu nakuhitaji vivyo kila saa! Niwezeshe, Mwokozi nakujia. 2. Nina haja nawe; kaa nami, na maonjo haya, hayaumi. Yesu nakuhitaji … 3. Nina haja nawe, kila hali, maisha ni bure, ukiwa mbali, Yesu nakuhitaji … 4. Nina haja nawe, nifundishe na ahadi zako zitimize. Yesu nakuhitaji … 5. Nina haja nawe, mweza yote, ni wako kabisa siku zote. Yesu nakuhitaji …
1. Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Muumbaji mbingu na dunia. Atukuzwaye pote umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote. 2. Mungu wake Yakobo, ndiye Mungu wetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema, unacho kitu chema, umepata mali; moyo utakung’aa shida zitakwisha. 3. Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye, kwa hekima aumba, vyote ni ajabu, misitu na mabonde, milima, mashamba, vilivyo baharini wanyama porini. 4. Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili: ...
1. Mganga wetu ni karibu, hashindwi na uchawi, upendo wa kutufia ni dawa yake njema: Imbeni na malaika, Jina lenye furaha, ndilo la kutukuka, Jina lake Yesu. 2. Hatuna utengamano wala uzima hata, ila Yeye kweli ndiye aliyetupumzisha: Imbeni … 3. Machukio na ugomvi ametuondolea, twende na kumtegemea hata kwake mbinguni: Imbeni … 4. Hulioni Jina tamu lake Mwokozi Bwana? Atuletea wokovu, hatashindwa na kufa: Imbeni … 5. Hilo ndilo nipendalo, linipalo uzima, ...
Comments
Post a Comment