304. Nitakupenda Nguvu Yangu
1. Nitakupenda nguvu yangu
nitakupenda Mwokozi,
nitakupenda nikitenda
mambo yakupendezayo,
nitakupenda nuru kuu,
kwa nguvu za moyo.
2. Nitakupenda ee rafiki
uzima wangu wa kweli.
Nitakupenda na kusifu,
nionapo mwanga wako.
Nitakupenda, Mwokozi
Kondoo wa Mungu.
3. Nimechelewa Bwana wangu,
kukufuata vizuri;
sikukujua siku nyingi,
uliye raha ya moyo.
Lakini sasa najuta
nitakufuata.
4. Nakushukuru jua langu,
waning’aza moyo wangu;
nakushukuru Bwana wangu,
uliyenipa uhuru;
nakushukuru Mwokozi
uliyeniponya.
5. Unipe nguvu ya kudumu
nisikuache kabisa;
uniongoze siku zote
nisianguke njiani,
ung’aze mwili na roho
kwa nuru ya mbingu.
6. Nitakupenda taji yangu
nikiwa mwenye furaha;
nitakupenda Mponya wangu,
huzuni ikinitesa,
nitakupenda daima.
Yesu Bwana wangu.
Comments
Post a Comment