254. Ninataka Kumwimbia Mungu
1. Ninataka kumwimbia
Mungu kwa furaha kuu.
Ninaona kila siku
anihurumiavyo.
Moyo wake mwenye kweli
umejaa upendo tu,
abariki kwa wingi
wamtumikiao vema.
Vitu vyote vyaisha,
pendo lake milele.
2. Kama kuku alindavyo
watoto hatarini,
vivyo Baba anilinda
kila siku kwa nguvu.
Ndiye aliyeniumba
akanipa mwili huu
na uzima na roho
siku zote mpaka leo.
Vitu vyote …
3. Jinsi hii aliupenda
Mungu ulimwengu huu,
hata akamtoa Mwana,
kwa ajili ya watu.
Naye Yesu aliteswa
akafa pale mtini
atuokoe sisi.
Tazameni pendo hili!
Vitu vyote …
4. Roho wake Mtakatifu
ni kiongozi wangu,
aniangalia vema
niingie mbinguni.
Aning’aza moyo wangu
kwa tegemeo langu
limshindalo Shetani,
asiweze kunidhuru.
Vitu vyote …
5. Nikishikwa na huzuni
ninajua faraja:
Shida na mateso yote
mwisho yatageuka.
Baada ya kaskazi kali
yanakuja masika,
vivyo baada ya shida
napewa furaha kubwa.
Vitu vyote ...
6. Pendo lake haliishi
Neno hili ni kweli.
Basi mimi mtoto wake
ninamwomba Babangu:
Unihurumie mimi,
nikushike kwa nia,
nikupende daima,
niishipo duniani;
na halafu milele
nitakaa na wewe.
Comments
Post a Comment