260. Umsifu Mungu ee Roho Yangu

1. Umsifu Mungu ee roho yangu!

   Nitamsifu kila siku.

   Siku nikaazo duniani

   nitamwimbia Bwanangu. 

   Kanipa mwili na roho, 

   amestahili sifa kuu.

   Haleluya! Haleluya!


2. Wafalme wa humu duniani 

   ni watu wanaokufa.

   Baada ya kufa mashauri 

   yao yanavunjika kabisa. 

   Hakuna msaada kwa watu,

   Mungu wa juu ndiye mponya.

   Haleluya! Haleluya!


3. Asaidiwaye na Mungu Baba 

   ni mwenye shangwe za kweli.

   Huyu haachi kumtegemea, 

   ijapo shida zizidi. 

   Aongozwaye na Bwana,

   hakosi njia ya msaada.

   Haleluya! Haleluya!


4. Ndiye aliyeviumba vyote, 

   vilivyo juu hata chini.

   Shauri la Mungu

   linatendeka kila atufanyialo.

   Ni Mfalme wa ulimwengu,

   atawalaye vizuri!

   Haleluya! Haleluya!


5. Yeye apenda kusaidia 

   wote wateswao bure.

   Awashibisha wapate nguvu

   wanaoona njaa sana.

   Awafungua wafungwa, 

   anazo rehema nyingi. 

   Haleluya! Haleluya!


6. Enyi umati sifuni Bwana

   awatendeaye makuu. 

   Wenye uzima wamsifu sana

   na mashangilio mema. 

   Tumwimbiaye ni Mungu 

   Baba na Mwana na Roho. 

   Haleluya! Haleluya! 


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu