291. Yesu Awakubali Wakosa
1. Yesu awakubali
wakosa, wahalifu.
Waambieni wa mbali
habari ya wokovu.
Tangazeni kwa bidii,
akubali wakosa!
Liwe neno dhahiri,
akubali wakosa!
2. Awakubali Bwana
Neno lake amini,
watu kila aina,
waje kwake tengoni.
Tangazeni …
3. Mimi ni safi moyo
na mbele ya sheria.
Aliye safi roho
kwake ilitimia.
Tangazeni …
4. Akubali wakosa,
nami anikubali.
Alivyonitakasa
mbinguni nawasili.
Tangazeni …
Comments
Post a Comment