293. Kujua Yesu u Karibu

1. Kujua Yesu u karibu 

   kwanituliza moyo wangu 

   na kuona: Macho

   yako juu yangu kwaniletea 

   amani nyingi. Nakusifu.


2. Hatujaona uso wako 

   wenye upole na rehema, 

   lakini rohoni tunakujua, 

   tunafahamu huruma yako 

   na upendo.


3. Afikiriye mchana kutwa 

   kukufahamu na kujua,

   hupata furaha zisizokoma 

   kwa kuona: Hakuna aliye 

   kama wewe.


4. Kuvumilia wakosaji, 

   kutusamehe kila siku,

   kutufurahisha na kutuponya,

   kutufariji na kutubariki:

   Kazi yako.


5. Utuonyeshe wokovu huu, 

   wa kutuponya kila siku,

   ukaifundishe mioyo yetu 

   ikutukuze na kukupenda 

   siku zote.


6. Siku za shida tutulize 

   kwa kufa kwako msalabani,

   tukumbuke vema mateso yako 

   na kukushika kwa nguvu zote

   mioyoni.


7. Kwa njia hii tutafurahi

   kama watoto mpaka mwisho. 

   Na ikitupasa kuhuzunika 

   utufariji mioyo yetu, itulie.


8. Unatuonyesha makovu 

   uliyopata msalabani. 

   Nasi tukiona alama hizi

   hatuna budi kukushukuru 

   na kusifu.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu