289. Yesu Ndiwe Mponya Wetu

1. Yesu ndiwe Mponya wetu,

   ninakukimbilia,

   kwani simba hutafuta 

   atakavyotumeza.


2. Yesu kukutumaini,

   kunanipa moyo mkuu,

   nina shangwe nikuone 

   katika ufalme juu.


3. Yesu wewe nakushika,

   ijapo kwa unyonge, 

   kwa mwingine sina msaada, 

   nikubali, ee Yesu!


4. Yesu nisafishe roho,

   nipate kuja kwako, 

   wema wote niuone 

   na nikusujudie.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu