281. Kwa Nini Wataka Kungoja?

1. Kwa nini wataka kungoja?

   Ondoka upesi ndugu! 

   Mwokozi apenda kukupa

   pumziko na raha yake. 

        Mbona? Mbona? 

        Mbona hutaki kumjia? 

        Mbona? Mbona? 

        Mbona hupendi raha?


2. Ni faida gani kungoja? 

   Maisha yapita hima.

   Ni Yesu tu abarikiye, 

   kumshika yafaa sana.

         Mbona? …


3. Huvutwi moyoni ee ndugu,

   na roho yenye uzima?

   Hupendi kupata wokovu? 

   Hima umtafute Yesu. 

         Mbona? …


4. Kwa nini wataka kungoja?

   Kufa kwako ni karibu. 

   Milango ya mbingu i wazi, 

   njoo mfuate Yesu Bwana. 

         Mbona? …


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu