298. Kwa Huruma Nikubali
1. Kwa huruma nikubali
Yesu hivi nilivyo
niwe mali yako Bwana
Mwokozi mtakatifu.
Natafuta raha Bwana
nitaona kwako tu.
Nibariki, unilinde
niliye mtoto wako.
2. Nitakwenda njia zangu
nikikutumaini.
Unishike nisiweze
kukuacha daima.
Natafuta raha
Bwana…
3. Nikiona giza tupu
nipe nuru ya roho.
Niongoze kwenye giza
mwenye kweli na nuru.
Natafuta raha
Bwana…
4. Nitakupa moyo wangu,
nitaishi na wewe,
mpaka macho yawezapo
kuona uso wako.
Natafuta raha
Bwana...
Comments
Post a Comment