310. Ewe Mungu Ngome Yetu

1. Ewe Mungu ngome yetu 

   ya miaka mingi,

   Wewe u msaada wetu

   na ngao ya nguvu.

 

2. Chini ya kiti cha enzi 

   hatutaogopa,

   mkono wako wenye nguvu

   watusaidia.

 

3. Miaka elfu waona 

   kama siku moja,

   ndiwe Mungu wa milele,

   hukomi kabisa.

 

4. Maisha yetu yapita

   kama maji ya mto, 

   na rafiki yetu kama 

   ndoto ya usiku.

 

5. Ewe Mungu ngome yetu 

   ya miaka mingi,

   zifikishe roho zetu kwako

   juu mbinguni. 

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu