307. Yesu Mpenzi Wangu
1. Yesu mpenzi wangu
ufurahishaye
moyo kwa kweli.
Tangu siku nyingi
nina hamu kubwa
nawe Bwanangu.
Ndiwe mpenzi wangu mkuu,
Wewe peke yako Mponya
hapa duniani.
2. Wewe mlinzi wangu
waondoa shida zinitesazo.
Mwovu aogofye,
vyote viteteme,
Yesu yu kwangu.
Huzuni ikizidi,
vyote vikiharibika
Yesu anishika.
3. Nakataa furaha hata mali zote
za dunia hii.
Yesu mali yangu.
Yesu ni furaha ya moyo wangu.
Nikiachwa kabisa
na jamaa zangu wote,
sitamwacha Yesu.
4. Roho ya huzuni
nenda zako mbali, Yesu yuaja.
Yesu akiwapo, hata shida zote
hazinishindi.
Watu wakinitesa
hawawezi kunitenga
na Mwokozi wangu.
Comments
Post a Comment