258. Namtumaini Bwana Tu
1. Namtumaini Bwana tu
ndiye mtuliza moyo.
Amkimbiliaye huyu,
hatindikiwi nuru,
Kwa Neno la Bwana Mungu
roho itatulia,
moyo watengemana.
2. Kila anayekupenda
huona msaada wako,
akishikwa na mashaka,
utamtuliza moyo.
Moyoni mwa mpenda Mungu
hamu itatulia,
uchungu hutoweka.
3. Roho yangu usiache
kumtumaini Bwana!
Waelekevu huona;
kwake vituo vyema.
Bwana ndiye mwenye nguvu
katika shida zote;
ni kinga hatarini.
4. Mkononi mwako naweka
maisha na uzima.
Nakuinulia macho
niwapo duniani.
Baada ya siku hizi
ukanipe kukaa
mbinguni kwako Baba.
Comments
Post a Comment