279. Haleluya, Mshukuruni Bwana

1. Haleluya, mshukuruni Bwana

   kwenye kusanyiko la kweli.

   Na malaika waungana nasi

   kushukuru amani yake.

   Matendo yako, Bwana, 

   ni makubwa kwa wote,

        Kazi (Zakutukuza mno 

        zina utukufu)  

        zakutukuza (mno ee) 

        Bwana.


2. Haleluya, mtukuzeni Bwana,

   takatifu Jina la Bwana, 

   wateule duniani pote, 

   shangilieni upole wake. 

   Huruma zako Bwana,

   ni kubwa kwa wanao.

          Kazi …


3. Nchi zote, pokeeni neema,

   wokovu huu kwa watu wote.

   Kila mtu asikosekane

   kwenye lango la mji ule. 

   Tukiitwa majina, 

   tutaruka kwa shangwe. 

          Kazi ...


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu