248. Neno Lako Bwana ni Imara

1.  Neno lako Bwana ni imara sana; 

    hilo latuongoza, hilo latufunza.


2.  Adui wabaya wakikaribia,

    Neno lake Bwana ni ulinzi sana.


3.  Siku za dhoruba kesha ukiomba;

    Neno lake Bwana msaada sana.


4.  Ukiliamini, huenda na amani;

    una na furaha: Neno ni silaha.


5.  Ni furaha kweli, na wingi wa mali

    Neno lake Bwana kwa wasiokana.


6.  Neno la rehema, tungali wazima; 

    faraja i papo, tunapoagana.


7.  Tulijue sana Neno lako, Bwana,

    hapa tukupende kisha kwako twende.

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu