259. Yesu ni Rafiki Yetu
1. Yesu ni rafiki yetu
akaaye mbinguni.
Hutuombea kwa Baba,
na kutupatanisha,
lakini twajikosesha,
twajitwika mabaya,
tusipomtafuta Yeye
na kuomba kwa kweli.
2. Ukijaribiwa sana
ukiona mashaka,
usihangaike sana,
usikome kumwomba.
Yeye ni mwema kabisa
wa kutuhurumia,
atujua: Tu wanyonge;
husikia kuomba.
3. Ukipatwa na majonzi,
yakulemee sana,
moyo ukisikitika,
Yesu akusikia.
Watu wakikusimanga,
urushwe na dunia,
Yesu akukumbatia;
husikia kuomba!
4. Urafiki haukomi
kwao wampendezao.
Kwa hiyo na tujikaze kumpenda
Bwana Yesu.
Bwana Yesu ndiye Mfalme
awashindaye wote;
wote wamtumikiao
atawavika taji.
Comments
Post a Comment