278. Mshangilie Bwana
1. K: Mshangilie Bwana dunia yote, mshangilie
W: Bwana dunia yote.
2. K: Msifu Bwana na shangwe kubwa, msifuni
W: Bwana na shangwe kubwa.
3. K: Njooni mbele zake kwa nyimbo nzuri; njooni mbele
W:Zake kwa nyimbo nzuri.
4. K: Jueni kwmba Bwana ndiye Mungu, jueni
W:Kwamba Bwana ndiye Mungu.
5. K: Ndiye Muunba wetu, sisi watu wake; ndiye Muumba
W: Wetu, sisi watu wake.
6. K: Malishoni mwake atuongoza; malishoni
W: Mwake atuongoza.
7. K: Ingieni mwake kwa kumshukuru; ingieni
W: Mwake kwa kumshukuru.
8. K: nyuani mwake tumsifu sote; nyuani
W: Mwake tumsifu sote.
9. K: Na jina lake tulihimidi; na jina
W: Lake tulihimidi.
10. K: Bwana ndiye mwema siku zote kwetu, Bwana ndiye
W: Mwma siku zote kwetu.
11. K: rehema zake ni za milele; rehema
W: Zake ni za milele.
12. K: Uaminifu wake kwa vizazi vyote; uaminifu
W: Wake kwa vizazi vyote.
Comments
Post a Comment