299. Kwako ee Yesu, iko Furaha

1.  Kwako ee Yesu,

    iko furaha, 

    katika shida zote.

    Wewe watupa 

    mambo ya mbingu,

    ndiwe Mponya wa kweli.

    Watukomboa sisi watumwa.

    Akushikaye, atasimama 

    hata milele, Haleluya! 

    Tunakumbuka rehema zako,

    Tunakushika hata tukifa 

    hatukuachi, Haleluya!


2.  Tukikushika, mwovu na kufa

    hana nguvu juu yetu. 

    Wewe hodari kutukingia shida

    na msiba wote.

    Twakutukuza, twakuimbia, 

    tunazidisha heshima yako

    kwa nyimbo nzuri. Haleluya!

    Tuna furaha, twashangilia,

    twasifu sana nguvu ya Bwana

    hatutakoma.  Haleluya!


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu