267. Baba Yetu Aliye Mbinguni Amenifurahisha

1.  Baba yetu aliye mbinguni 

    amenifurahisha kwa kweli.

    Kaniambia rohoni mwangu

    Yesu yu nami, ananipenda. 

          Anipenda Yesu Mwokozi, 

          anipenda, anipenda. 

          Anipenda Yesu Mwokozi, 

          anipenda kweli.


2.  Nimwachapo nikaenda mbali, 

    Yeye yu vivyo, ananipenda.

    Akaniita kwake upesi,

    Yesu yu nami, ananipenda. 

             Anipenda …


3.  Anipenda, nami nampenda

    wokovu wangu ulipokuja. 

    Tukimwona kufani Golgota,

    Yesu yu nami, ananipenda. 

             Anipenda …


4.  Kujua haya kwanipa raha,

    kumtegemea kuna furaha.

    Amfukuzapo hivi Shetani,

    Yesu yu nami, ananipenda.

             Anipenda …


5.  Sifa ni nyingi asifiwazo,

    moja ni kubwa katika hizo. 

    Hata mbinguni nitamwimbia 

    Yesu yu nami ananipenda! 

              Anipenda …


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu