312. Nakuapia Yesu

1. Nakuapia Yesu kukutumikia

   Wewe u mfunzi wangu

   na rafiki mwema. 

   Sitaogopa vita nikikufuata 

   siipotezi njia ukiniongoza.


2. Dunia i karibu, Bwana unilinde,

   na majaribu mengi 

   yako pande zote.

   Adui siku zote ni ndani na nje, 

   Ee Yesu univute  karibu na Wewe!


3. Nazisikia sauti 

   zenye tamaa mbaya, 

   na mambo ya dunia 

   yanivuta sana. 

   Ee Bwana sema nami, 

   furaha iwe kuu, 

   nitakusikiliza,

   Wewe mlinzi wangu.


4. Waagana na wote wakufuatao,

   kwamba uliko Wewe, 

   nao watakuwa.

   Nami ninaagana kukutumikia,

   Yesu nisaidie  kukuandamia.


5. Hatua zako Bwana 

   naziona wazi,

   nizikanyage vema

   hapa duniani.

   Nishike hata mwisho,

   Ee Yesu Mwokozi, 

   nichukue nikifa 

   na kwako mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu