319. Yesu Unipendaye
1. Yesu unipendaye
kwako nakimbilia,
ni wewe utoshaye
mwovu akinijia;
yafiche ubavuni
mwako maisha yangu;
Nifikishe mbinguni,
wokoe moyo wangu.
2. Ngome nyingine sina,
Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana,
nipe neema yako,
ninakuandamia
mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia,
vitani wanitosha.
3. Nakutaka Mpaji
vyote napata kwako;
Niwapo mhitaji,
utanijaza vyako;
Nao waangukao
wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao.
Uongoze vipofu.
4. Bwana umeniosha
moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha
yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona,
kisima cha uzima:
mwangu moyoni, Bwana,
bubujika daima.
Comments
Post a Comment