287. Mwamba Wangu wa Kale

1.  Mwamba wangu wa kale,

    kwako nitajificha. 

    Maji na damu yako

    toka mbavuni mwako 

    ziwe dawa ya dhambi, 

    kutakasa mioyo.


2.  Si kazi ya mikono 

    iletayo wokovu. 

    Nikitoa machozi, 

    nikifanya na bidii

    siwezi kujiosha, 

    unioshe wewe tu.


3.  Mkononi sina kitu,

    ila msalaba wako,

    ni mtupu, nipe nguo;

    ni mnyonge, nipe nguvu;

    niondolee taka, 

    nitakase sijafa.


4.  Nikaapo duniani,

    nifikapo kifoni, 

    nitakapofufuka, 

    nitakapokuona;

    Mwamba wangu wa kale,

    kwako nitajificha!

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu