266. Pote Atawala Nani?
1. K: Pote atawala nani?
W: Pote atawala nani?
K: Ni nani?
W: Ndiye Mungu Mwenyezi.
2. K: Msifuni Mungu wetu,
W: Msifuni Mungu wetu
K: Yu Bwana,
W: Vyote ni mali yake.
3. K: Mwumba jua nao mwezi,
W: Mwumba jua nao mwezi?
K: Na nyota
W: Kwani anayo enzi.
4. K: Sasa wewe roho yangu,
W: Sasa wewe roho yangu
K: Kubali,
W: Nyenyekea kwa Mungu.
5. K: Roho isiyotulia,
W: Roho isiyotulia,
K: Na Bwana,
W: Haitapata raha.
6. K: Amemtuma Mwana wake,
W: Amemtuma Mwana wake,
K: Yesu Kristo,
W: Ili atuokoe.
7. K: Amemshinda shetani,
W: Amemshinda Shetani,
K: Na dhambi,
W: Na kutupa uzima.
8. K: Asimamisha agano
W: Asimamisha agano,
K: La Bwana,
W: Haleluya, ee Yesu.
9. K: Dunia wamsifu,
W: Dunia wamsifu
K: Kwa shangwe,
W: Kwa kuwa hututunza.
10. K: Watawala na raia,
W: Watawala na raia,
K: Na waje,
W: Wamshukuru Mwokozi.
11. K: Tumsifu Mungu Baba,
W: Tumsifu Mungu Baba,
K: Na Mwana
W: Na Roho Mtakatifu.
12. K: Yatupasa kushukuru,
W: Yatupasa kushukuru
K: Upendo,
W: Ulio wa milele.
Comments
Post a Comment