313. Kwa Neema na Pendo
1. Kwa neema na pendo
ameniweka huru,
si ustahili wangu,
si haki na matendo.
/: Ni Yesu, Bwana
wangu,
Kwa neema ’meniweka
huru./:
2. Kwa moyo wa ubaba
ameniweka huru,
si kwa sababu zangu,
si kwa ujuzi wangu.
Ni Yesu, …
3. Kwa utakaso wake
amesamehe yote;
Amefuta madeni
na dhambi na ujinga.
Ni Yesu, …
4. Kwa damu ya thamani
amelipia yote;
Na vyeti vya madai
amepasua vyote,
Ni Yesu …
5. Kwa ukubali wake
amekubali wote:
Wenye mizigo wote
huwapumzisha vema.
Ni Yesu, …
6. Ijapo dhambi zenu
nyekundu kama damu;
Kwa damu takatifu
na iwe kama pamba.
Ni Yesu, …
7. Kwa neema na pendo
amejitoa kwangu!
Mimi na nyumba yangu
tunajitoa kwake.
Ni Yesu, …
Comments
Post a Comment