297. Kuna Chemchem Itokayo
1. Kuna chemchemi itokayo
damu ya wokovu.
Chemchemi itendayo makuu
na kutufariji.
2. Shida zangu zinakwisha
zote kwa damu hii,
kwani Yesu amekufa
kwa ajili yangu.
3. Mwana Kondoo damu
yako inayo nguvu kuu.
Tupe roho wako Bwana,
Tuwe watu wapya.
4. Nami mwenye dhambi
nyingi nimekombolewa.
Kwa damu hii ya Mwokozi,
namsifu Yeye tu.
5. Damu hii inanipa
furaha ya kweli.
Sababu hii nitamsifu
Mwokozi daima.
Comments
Post a Comment