269. Ni Wako Wewe, Nimekujua
1. Ni wako wewe, nimekujua
na umeniambia:
Lakini Bwana, nataka kwako
nizidi kusogea:
Bwana vuta, (vuta)
nije nisogee sana
kwako mtini.
Bwana vuta,
vuta nije nisogee
pa damu ya thamani.
2. Niweke sasa nikatumike
kwa nguvu za neema.
Uyapendayo nami nipende
nizidi kukwandama:
Bwana vuta …
3. Nina furaha tele kila saa
nizungumzapo kwako,
nikuombapo, nami napata
kujua nia yako:
Bwana vuta, …
4. Mapenzi yako hayapimiki
ila ng’ambo yaliko
anasa pia sitazijua
bila kufika kwako
Bwana vuta,…
Comments
Post a Comment