288. Masikini Bartimayo
1. Masikini Bartimayo
alikaa njiani,
alikuwa akiomba
haja za kimwili.
2. Akasikia sauti kuu
ya jeshi la watu,
akauliza upesi:
Kuna nini ndugu?
3. Ndiye Yesu Mnazareti,
anapita sasa.
Papo hapo Bartimayo
akaita sana.
4. Ee Yesu, mwana Daudi,
mimi nakuomba,
sasa unihurumie
kipofu, masikini!
5. Bwana Yesu kwa huruma
akamwita aje. Sema:
Watakani kwangu?
Nikufanyieje?
6. Mimi Bwana ni kipofu,
nataka nione,
nakuomba sana Bwana
unihurumie!
7. Na Yesu akamwambia:
Nenda zako sasa.
Imani inakuponya!
Mara akaona.
8. Sote tu vipofu Bwana
utuhurumie!
Macho yetu yafumbue,
Na tukufuate!
Comments
Post a Comment