285. Nilikuwa Kondoo

1.  Mimi ni mtu mkosaji, 

    ni mwenye moyo mnyonge,

    mwenye uchafu mwingi.

    Mungu nihurumie!


2.  Wema sina kabisa,

    lakini maovu tu, 

    nimepunguka sana.

    Mungu nihurumie!


3.  Moyo umevunjika,

    nina woga kwa macho 

    kutazama mbinguni. 

    Mungu nihurumie!


4.  Yuko mmoja mbinguni, 

    ndiye mwokozi wetu,  

    nami ninamngojea. 

    Mungu nihurumie!


5.  Niliyemtegemea, 

    Yeye hatanitupa, 

    anipenda kwa moyo.

    Mungu nihurumie! 

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu