284. Ninakulilia Mungu
1. Ninakulilia Mungu
katika shida kubwa.
Usikilize maombi
na sala kwa rehema.
Kwani ukiyahesabu
makosa yetu na dhambi,
aponaye ni nani?
2. Inatupasa rehema
tuondoshwe mabaya.
Kutenda kwetu ni bure,
tujapofanya mema.
Hakuna anayeweza
kujisifu mbele yako,
wataka tu huruma.
3. Sababu hii inanifaa
kumtumaini Mungu;
rehema yake ni kubwa
aliyoniwekea.
Nashika Neno lake tu
lenye tulizo kubwa mno;
Mungu ana rehema.
4. Nikiwa na shida nyingi
sababu ya makosa.
Sishindwi nazo, siachi
kumtumaini Mungu.
Wakristo wa kweli wote
wanafuata njia hii,
kungoja saa ya Mungu.
5. Dhambi zetu nyingi sana
hazishindi rehema.
Mungu ni mweye nguvu kuu
za kuzifuta zote.
Mchungaji mwema ni yeye
atakayetuokoa tutoke
makosani.
Comments
Post a Comment