253. Nakuimbia Wewe Bwana
1. Nakuimbia wewe Bwana
hakuna mwingine kama wewe.
Nakuimbia nyimbo zangu,
unipe nguvu ya roho wako,
anifundishe nyimbo za sifa,
niziimbe kwa Jina la Yesu.
2. Baba nivute kwa Mwanao,
Mwanao anivute na kwako.
Mtakatifu uniongoze,
mawazo yangu yawe mazuri.
Amani yako ikae mwangu,
nikuimbie kwa furaha kuu.
3. Ukinisaidia hivi,
Bwanangu nitaweza kuimba
kukusifu wewe vizuri
kwa roho na kwa kweli kila saa.
Maana Roho anaongoza
niimbe malaika waimbavyo.
4. Naomba nilivyofundishwa
na Roho wako yakupendeze.
Nawe unasikia yote
sababu ya Mwana wako Yesu,
aliyenifanya mtoto wako
na mrithi wa ufalme wa mbingu.
5. Ni heri nikijua haya!
Naweza kukuomba vizuri:
Najua kila kitu chema
nitakachoomba nitapewa,
sababu kila kipaji chema
kinashuka kutoka kwa Baba.
6. Naomba kwa Jina la Yesu
aniombeaye kwake Mungu.
Lolote nitakaloomba
kwa Jina lake Bwana anipa.
Sababu hii nakusifu Bwana,
nakushukuru kwa nyimbo zangu.
Comments
Post a Comment