272. Twakuomba, ee Baba Mungu
K: Twakuomba, Ee Baba Mungu,
tupe rehema ya kimbingu;
Tuwe watu wa Mungu.
W: Wa utukufu.
1. W: Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako tutalitukuza,
mapenzi yako ni ya makini
mbinguni na duniani.
2. K: Tupe leo riziki yetu,
tusamehe makosa yetu
kama sisi tunavyosamehe
wanaotukosea.
3. W: Usitutie majaribuni,
Tuokoe na yule mwovu,
kwani wako ndio ufalme
sasa na hata milele.
K: /: Utukufu ni wako
W: Hata milele:
K: Utukufu ni wako
W: Hata milele.
K: Utukufu ni wako
W: Hata milele.
K: Utukufu milele Amen:/
Comments
Post a Comment