262. Tumshukuru Mungu
1. Tumshukuru Mungu
kwa kinywa na kwa moyo,
atendaye makuu
popote hata kwetu.
Tangu kuzaliwa
mpaka leo hivi na siku
zijazo hutuhurumia.
2. Baba mwenye nguvu
atupe siku zote mioyoni mwetu
furaha na amani.
Baraka yake kuu itusaidie,
tushinde huzuni na shida zozote.
3. Tumsifu Mwenyezi
aliye Baba yetu,
Tumsifu na Mwana aliyetuokoa.
Tumsifu na Roho
atutakasaye.
Tumsifuni Mungu
sasa na milele.
Comments
Post a Comment