255. Tuwe na Raha Moyoni
1. Tuwe na raha moyoni
na kujazwa shukrani,
kwani Baba wa mbinguni
atutaja watoto.
Daima tutafurahi,
kila siku ni jua.
Njia ya uzima nzuri
sana, tufurahi milele!
2. Mungu anatuongoza
ni tegemeo letu,
huruma yake hutupa
nguvu ya kila siku.
Daima tutafurahi …
3. Tunapojitenga naye,
giza latuzunguka,
mwendo wetu si imara
hamna raha moyoni.
Daima tutafurahi …
4. Waongofu huchipushwa,
njia zao mwanga tu.
Na tumtumikie Yesu
Tukatae kukosa.
Daima tutafurahi …
Comments
Post a Comment