295. Mungu Amenihurumia
1. Mungu amenihurumia,
tendo hili kubwa sana.
Sikustahili jambo hili
nimelipata bure tu.
/: Sasa najua haya yote,/:
nasifu huruma yake.:/
2. Nalistahili kupotea,
lakini nahurumiwa.
Mungu amenipatanisha
na Yeye kwa Yesu Kristo.
/: Hivi vyote vyatoka
wapi?:/
/: Nasema ni huruma
tu:/
3. Jambo hili lenye huruma
nitalisifu daima.
Nalihubiri siku zote,
nikiulizwa na watu.
/: Ndilo furaha yangu
kubwa,:/
/: nalingojea, nikifa. :/
4. Huruma hii ni kubwa sana,
nitaisifu daima.
Naitafuta nikiomba
nategemea hiyo tu.
/: Sababu hii navumilia,:/
/: naingojea, nikifa. :/
5. Mungu mwenye huruma nyingi
usininyime huruma.
Mimi ni mkiwa, nipeleke
kwako kwa kufa kwa Yesu.
/: Kule mbinguni nitasifu,:/
/: huruma yako milele. :/
Comments
Post a Comment