275. Tumwimbie Bwana
1. K: Tumwimbie Bwana,
W: Maana ndiye,
mwamba wa wokovu
wetu.
2. K: Tuje mbele zake,
W: Tumfanyie
Yeye shangwe kwa
Zaburi.
3. K: Bwana ndiye Mungu
W: Na Mfalme
Mkuu juu ya miungu
yote.
4. K: Mkononi mwake,
W: Yamo mabonde
na milima ya dunia.
5. K: Bahari ni yake,
W: Aliiumba
pamoja na nchi kavu.
6. K: Njooni tumwabudu,
W: Tumpigie
magoti aliyetuumba.
7. K: Ndiye Mungu wetu,
W: Na sisi ndio
watu wa malisho yake.
8. K: Na kondoo wake,
W: Ni heri kusikia
sauti yake leo.
9. K: Msijishupaze,
W: Kama huko Meriba
na siku ya Masa.
10. K: Ndipo Baba zenu,
W: Walinijaribu sana
kule jangwani.
11. K: Nalihuzunika
W: Kwa vile wasivyozijua
njia zangu.
12. K: Nalijiapia,
W: Hawataingia kamwe
rahani mwangu.
13. K: Atukuzwe Mungu,
W: Baba na Mwana
na Roho Mtakatifu
14. K: Jinsi ‘livyokuwa
W: Mwanzo na sasa
na hata milele, Amen.
Comments
Post a Comment