303. Neno Moja Bora Sana

1. Neno moja bora sana,

   lishindalo mengine.

   Mambo yote ya dunia 

   ndiyo mzigo mzito tu,

   unaotutesa miili na roho,

   lakini hayatunyang’anyi furaha.

   Nikiwa na moja lililo bora 

   naona furaha isiyoisha.


2. Roho ukitaka hili,

   hulioni kwa watu.

   Acha mambo ya dunia, 

   hima nenda mbinguni, 

   alipo Mwokozi 

   pamoja na Mungu,

   palipo na nguvu  

   na haki na kweli,

   ndipo utakapoliona lile 

   linalokupasa hapa na huko.

 

3. Kumbuka Maria pale 

   miguuni pa Yesu. 

   Alivyosikia Neno alilohubiriwa.

   Hakuna jingine alilolipenda 

   kuliko maneno ya 

   Yesu Mwokozi; 

   hakuna mawazo aliyowaza

   kuliko kumwona na kumsikia.


4. Hivyo hata moyo wangu 

   unamtaka Yesu tu. 

   Unisaidie Bwana, 

   nikushike daima.

   Naona wengine wapenda dunia, 

   na mimi napenda tu kukufuata.

   Neno lako Yesu lenye uzima,

   lanipa furaha isiyoisha.


5. Moyo wangu unaona 

   raha na amani tu. 

   Kwani Yesu Mchunga 

   wangu anilisha vizuri. 

   Sijui furaha ipitayo hii 

   ya kuwa na Yesu 

   na kumtumikia.

   Sijui yawezayo kunitosha 

   kuliko kumshika 

   kwa nguvu zote.


6. Yesu wewe peke yako 

   u hazina yangu kuu. 

   Utazame moyo wangu, 

   unafiki ung’oe.

   Nionye, nikiwa katika hatari

   ukaniongoze nipate uzima. 

   Nijue: Dunia ni taka tupu, 

   kumjua Mwokozi ni neno bora.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu