277. Leo Siku ya Mungu
1. Leo siku ya Mungu,
tuko mbele zake.
Jambo kubwa tuabudu
na kusujudia.
/: Sasa tutulie
mbele zake Mungu.
Awe nasi sote
mioyoni mwetu. :/
2. Sisi viumbe vyake
tuombe huruma,
Muumba vitu vyote
atuhurumie.
/: Yeye atupenda
na kujua yote.
Manza zetu zote
atazisafisha. :/
3. Neno lake la leo
liwe ndani yetu.
Mapenzi yake yote
yatimizwe kwetu.
/: Tumfuate yeye,
na tuishi naye.
Awe baba yetu
maishani mwetu. :/
4. Sisi wana wa Mungu,
tuna hamu kubwa
kuwa na neema yake.
Yesu Bwana wetu.
/: Basi, ndugu sote,
tuwe ndani yake,
naye ndani yetu,
tumtumikie. :/
Comments
Post a Comment