317. Cha Kutumaini Sina

1.  Cha kutumaini sina 

    ila damu yake Bwana,

    sina wema wa kutosha

    dhambi zangu kuziosha;

           Kwake Yesu nasimama, 

           ndiye Mwamba ni salama 

           ndiye Mwamba ni salama.


2.  Njia yangu iwe ndefu 

    Yeye hunipa wokovu; 

    Mawimbi yakinipiga 

    nguvu zake ndiyo nanga.

             Kwake Yesu …


3.  Damu yake na sadaka 

    nategemea daima, 

    yote chini yakiisha

    Mwokozi atanitosha. 

               Kwake Yesu …


4.  Nikiitwa hukumuni,

    rohoni nina amani; 

    Nikivikwa haki yake

    sina hofu mbele zake. 

               Kwake Yesu …

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu