315. Bwana ni Nuru na Wokovu Wangu
1. K: Bwana ni nuru
na wokovu wangu,
W: Ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani duniani?
2. K: Watenda mabaya
walinijia,
W: Wanile nyama yangu yote,
Wakajikwaa wakaanguka.
3. K: Jeshi likijipanga tupigane,
W: Moyo wangu hauogopi,
vita vijaponitokea.
4. K: Hata hapo ninalo tumaini;
W: Neno moja nataka, Bwana,
ndilo ninalolitafuta.
5. K: Nikae nyumbani
mwa Bwana wangu,
W: Siku zote maisha yangu,
nione uso wake Bwana.
6. K: Niutazame uzuri
wa Bwana.
W: Nikae hekaluni mwake,
nitafakari mema yake
7. K: Atanilinda siku ya mabaya,
W: Hunificha hemani mwake,
huniinua juu ya mwamba.
8. K: Sasa kichwa changu
kitainuka,
W: Juu yao adui zangu.
Wajaponizunguka kote.
9. K: Nitazitoa dhabihu
za shangwe;
W: Hemani mwake
nitaimba, naam,
nitamtukuza Bwana.
Comments
Post a Comment