290. Wakosaji Fikirini
1. Wakosaji fikirini
mwisho wa njia zenu!
Hamwogopi kupotezwa
vibaya kuzimuni?
Rudini kwake Mwokozi!
Ndiye mwenye huruma,
hawatupi wamjiao,
njooni tu kwake Yesu!
2. Hapo mlipoyafuata
mambo ya dunia hii,
hamkuweza kuvivunja
vifungo vya Shetani.
Rudini kwake …
3. Mambo yote hugeuka,
tukimjua Mwokozi;
twaondolewa makosa,
tuwe wake Bwana tu.
Rudini kwake …
4. Wote wampendao Bwana
huwagawia mema;
njooni nanyi myapokee
hayo mema ya mbingu!
Rudini kwake …
5. Mpokeeni mioyoni
hamwezi kujilinda!
Lakini akiwatia
nguvu zake mwapona.
Rudini kwake …
6. Njooni na kumwangukia,
awaokoe nanyi!
Atawapokea vema,
msifuni siku zote.
Rudini kwake …
Comments
Post a Comment