283. Bwana Yesu Wapi?

1.  Bwana Yesu yuko wapi,

    mpenzi wangu rafiki? 

    Njia gani amekwenda? 

    Nitamwonaje mimi? 

    Roho yangu yajutishwa

    na dhambi na huzuni; 

    Yesu mpenzi wangu mwema 

    namtafuta kwa bidii.


2.  Ninapaza sauti yangu 

    nalia: Wapi Yesu? 

    Ndani mwangu sina raha

    mpaka nimwone Yesu. 

    Ningekuwa na mabawa 

    ningeruka upesi

    milimani, mabondeni

    kumtafuta Bwanangu.


3.  Aondoa shida zangu, 

    maharibifu yote. 

    Nikiona taabu mimi 

    anituliza yeye.

    Nitafanya bidii sana;

    kumtafuta popote; 

    sitachoka kutembea 

    mchana hata usiku.


4.  Bwana Yesu nitokee,

    roho inakuita. 

    Niondoe na maovu 

    Yesu Mwokozi wangu. 

    Utulize hamu yangu  

    kaa kwangu daima. 

    Nikupende sana wewe, 

    niwe wako milele.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu