305. Unishike! Mimi ni Mnyonge
1. Unishike!
Mimi ni mnyonge sana
siwezi kwenda pasipo Wewe.
Unishike!
Uliye Mponya wangu,
hofu na taabu hainishindi.
2. Unishike! Ukanivute kwako,
niwe karibu na moyo wako.
Unishike! Kwani nakosa njia
nzuri nikienda peke yangu.
3. Unishike! Naona giza tupu
nisipouona uso wako.
Lakini nuru yako iking’aza
njia yangu naona furaha.
4. Unishike! Utakaponiita niende
kulazwa kaburini.
Mwanga wako utokao
mbinguni
uning’azie njia ya mwisho.
Comments
Post a Comment